Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumzia unyanyapaa dunia inapoadhimisha siku ya ugonjwa wa mtindio wa ubongo

Ban azungumzia unyanyapaa dunia inapoadhimisha siku ya ugonjwa wa mtindio wa ubongo

Katika kuadhimisha siku ya  mtindio wa ubongo  duniani  ambayo huadhimishwa Machi 21 kila mwaka, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema unyanyapaa dhidi ya watu wenye ulemavu huo huwanyima nafasi nyingi.

Ugonjwa wa mtindio wa ubongo (Down Syndrome) ni hali ya kiasili inayotokea kwa mwili wa mwanadamu inayoathiri uwezo wa kujifunza, tabia za kawaida na afya. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya ukuaji na maendeleo ya  kiumbe unategemea afya bora, kujumuishwa katika elimu na  kufanyiwa utafiti yakinifu.

Bwana Ban amesema katika sehemu za kazi, ubaguzi dhidi ya watu wenye mtindio wa ubongo mara nyingi husababisha kukosa fursa za mafunzo ya stadi za kazi na kukosa haki ya kufanya kazi. Ameongeza kuwa katika nyanja za kisiasa na kijamii, watu wenye ulemavu wa akili  huwa wananyanga’nywa haki ya kupiga kura na kushiriki katika mchakato mzima wa demokrasia.