Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kukabiliana na usafirishaji binadamu

IOM kukabiliana na usafirishaji binadamu

Kwa mujibu wa takwimu za idara ya Umoja wa Mataifa dhidi ya mihadarati na uhalifu duniani, UNODC, biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu  ni ya pili kwa pato la juu la fedha haramu  nyuma ya biashara ya mihadarati. Kwa mwaka biashara hii huingiza fedha haramu kiasi cha dola za Kimarekani bilioni thelathini na moja .

Aidha utafiti wa Shirika la Kimtaifa la Uhamiaji, IOM nchini Ethiopia unaitaja nchi hiyo kama miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa usafirishaji haramu wa binadamu ambapo raia wa nchi hiyo, wengi wao wakiwa ni wanawake, husafirishwa kwa mwaka.

Katika kukabiliana na biashara hiyo inayoukuwa kwa kasi ulimwenguni, IOM imetiliana saini mkataba wa maelewano na Ethiopia wenye lengo la kuiwezesha nchi hiyo kuzuia biashara haramu ya usafirishwaji wa wanadamu. Serikali ya Marekani imetoa msaada wa dola elfu tano ili kuwezesha mradi huu.

Joseph Msami amefanya mahojiano na msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe  kufahamu undani wa mkataba huo, na hapa Jumbe anaanza kwa kueleza hatua za awali zilizochukuliwa na serikali ya Ethiopia na namna IOM itakavyowezesha serikali ya Ethiopa  katika kudhibiti uhalifu huo wa kimataifa.

SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE