Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usafirishaji haramu binadamu Ethiopia wamulikwa: IOM

Usafirishaji haramu binadamu Ethiopia wamulikwa: IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Ethiopia wametia sahihi makubaliano ya kutekelezwa kwa mradi wa miaka miwili wenye lengo la kuzuia usafirishaji  haramu wa watu, kuwahakikishia usalama waathirika wa vitendo hivyo na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika nchini Ethiopia. Makubaliano hayo yalitiwa sahihi mjini Addis Ababa ambapo Jumbe Omari Jumbe msemaji wa IOM anafafanua zaidi kilichomo ndani ya makubaliano hayo.

(SAUTI YA JUMBE)