Kuelekea 2015, nishati mbadala yamulikwa Afrika:UNDP

19 Machi 2013

Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP leo limeanzisha majadiliano kwa kanda ya afrika kwa ajili ya kuanzisha msukumo mpya unaotaka kuIngizwa kwa kipengele kinachozingatia nishati mbadala wakati huu wa kuelekea kwenye kilele cha maendeleo ya maendeleo ya milenia, MGDs.  Majadiliano hayo ambayo yamewajumusiha maafisa wa serikali, wachumi, mashirika ya kiraia, yamefanyika jijini Dar es salaam, yakitanguliwa na majadiliano mengine yaliyofanyika hivi karibuni, India  kwa ajili ya nchi za Asia. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE)

Kukamilika kwa majadiliano hayo kutafungua njia kwa majadiliano mengine ya kimataifa yaliyopangwa kufanyika baadaye mwaka huko nchini Norway amajadiliano ambayo yatatoa mwanga kamaili kama agenda ya Umoja wa Mataifa kuingizwa kipengele kichozingatia nishati mbadili itakuwa imefaulu au la.  Wakati  huu lakini Umoja wa Mataifa unaendelea kuyapigia debe malengo ya maelendeleo ya mellenia ambayo yamegawika katika mikondo mbalimbali, ikiwemo utokomezaji umaskini na njaa, kupunguza vifo vya watoto wadogo na kina mama wakati wa kujifungua. Pamoja na kuwepo kw ahatua kubwa kwa baadhi ya malengo, hata hivyo Umoja wa Mataifa unaonakuwa wakati mwaka 2015 ukikaribia kuna baadhi ya maeneo bado hajapiga hatua, na hivyo kusudia la kuanzisha agenda ya ushirikishwaji wa nishati mbadala imelenga kusuka mbele kile kinachoitwa maendeleo endelevu.

Akizungumzia umuhimu wa kuweka mipango ya kuimarisha sekta ya nishati na madini, Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou alitoa mwito wa kuwepo kwa mashirikiano ya kikanda ili hatimaye kuwa na usemi mmoja . Kwa upande mwingine,Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo amesema kuwa, amesema kuwa bara la afrika limeadhimia kuondokana na utegemezi wa uzalishaji nishati ya umeme kwa kutumia vyanzo vya kale. Maazimio yaliyofikiwa kwenye majadiliano hayo yanakusudiwa kufikishwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter