WFP na UNHCR yapokea msaada kwa ajili ya kambi ya Nyarugusu

18 Machi 2013

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la wakimbizi UNHCR na lile la Mpango wa Chakula duniani WFP yamepokea msaada wa Dola Milioni Saba kutoka serikali ya Japan  kwa ajili ya kambi ya Nyarugusu iliyoko wilaya ya Kasulu, Kigoma, magharibi mwa Tanzania.

Kambi hiyo ni ya mwisho miongoni mwa kambi zinazohifadhi wakimbizi kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

Mellanie Senelle ni msemaji wa UNHCR na amefafanua matumizi ya msaada huo ikiwemo kuimarisha lishe bora.

SAUTI (MELLANIE)

‘‘Msaada huu toka Japan utasaidia wakimbizi katika maeneo muhimu ya afya ya msingi kama vile maji,malazi,lakini pia kuna malengo muhimu ya kielimu kuwasaidia watoto kujiunga elimu ya msing, .Pia tutasaidia wakimbizi wenye mahitaji maalum kama wazee,walemavu,wenye magonjwa sugu na wajawazito.’’

Halikadhalika msemaji huyo wa UNHCR amezungumzia namna UNHCR itakavyosaidia waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi katika kambi ya Nyarugusu

(SAUTI YA MELLANIE)

‘’UNHCR inafanya kazi na washirika wengine ambao wamejikita katika masuala ya   afya kama HIV, masuala ya elimu ya kinga,na kubadili tabia. Kwa hiyo msaada huu tutautumia kuboresha maisha ya waathirika wa ugonjwa hu’’.  

 

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter