Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Mali wahitaji msaada wa haraka: WFP

Wakimbizi wa Mali wahitaji msaada wa haraka: WFP

Wananchi wa Mali wanaendelea kuhangaika baada ya kupoteza makazi yao na kwa sasa wanahitaji haraka msaada wa chakula na misaada mingine ya kibinadamu. Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, Ertharin Cousin aliyoitoa mjini Roma baada ya kuhitimisha ziara yake huko Mali na Burkina Faso. Wakati wa ziara hiyio alijionea hali halisi ikiwemo kukutana na watu walioathiriwa na mzozo wa Mali pamoja na mfululizo wa ukame na mavuno duni. Maelezo zaidi kutoka kwa George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE)