Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wamulikwa teknolojia ya mawasiliano baada ya 2015.

Wanawake wamulikwa teknolojia ya mawasiliano baada ya 2015.

Tume ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uendelezaji wa teknolojia ya digitali imeweka lengo jipya la kuchochea wanawake kutumia zaidi teknolojia ya habari na mawasiliano, ICT kama njia mojawapo ya kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia yanayohusiana na jinsia.  Lengo hilo limewekwa wakati wa mkutano wa Saba wa makamishna wa tume hiyo huko Mexico City, Mexico.  Kwa mujibu wa mkutano huo, lengo hilo linataja kuwa ni lazima ifikapo mwaka 2020 kuwepo na usawa wa kijinsia katika matumizi ya mfumo wa kasi zaidi wa mawasiliano ya intaneti.   Kwa mujibu wa shirika la mawasiliano duniani, ITU, hivi sasa kwenye nchi zinazoendelea, wanawake wana nafasi finyu zaidi kulinganisha na wanaume katika matumizi ya teknolojia ya mawasiliano.  ITU  inasema katika nchi zilizoendelea pengo hilo lipo lakini ni kidogo ikiliganishwa na nchi zinazoendelea.