Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali za barabarani zamulikwa katika ripoti ya WHO

Ajali za barabarani zamulikwa katika ripoti ya WHO

Shirika la afya duniani WHO limetoa ripoti mpya inayoonyesha kuwa ni mataifa 28 tu yenye asilimia saba ya watu wote duniani ambayo yana sheria madhubuti za usalama barabarani kwenye maeneo makuu matano ambayo ni muhimu  katika kupunguza ajali za barabarani. Je, ni nini sura ya bara la Afrika katika viwango vya ajali na usalama barabarani?

Ungana na Joseph Msami katika tarifa hii inayoangazia ripoti hiyo na mikakati ya kujikinga na ajali hizo zinazotajwa kupoteza maisha ya mamilioni ya watu duniani, wengi wao wakiwa kutoka Afrika