Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Flavia Pansieri wa Italia kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu

Ban amteua Flavia Pansieri wa Italia kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amemteua Bi Flavia Pansieri, raia wa Italia, kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa.

Bi Pansieri atamrithi Bi Kyung-wha Kanga, ambaye Bwana Ban na Kamishna Mkuu Navi Pillay wamemshukuru kwa huduma yake ya miaka sita kwa mpango wa haki za binadamu Umoja wa Mataifa.

Bi Pansieri, ambaye alianza kufanya kazi na Umoja wa Mataifa mwaka 1983, amekuwa akihudumu kama Mratibu Mkuu wa mpango wa Kujitolea katika Umoja wa Mataifa (UNV).