Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji Afrika Magharibi na Kati

IOM kutoa mafunzo kwa maafisa Uhamiaji Afrika Magharibi na Kati

Maafisa waandamizi wa uhamiaji na askari kutoka nchi 13 zinazozungumza Kifaransa Magharibi na Kati mwa Afrika, wanakutana Jumatatu mjini Dakar Senegal kujadili njia bora za kupambana na uhamiaji haramu na namna ya kuwalinda wahamiaji walioko katika mazingira magumu.  Mafunzo hayo ni sehemu ya ufadhili wa mradi Shirika la Kimataifa la Uhamiaji ukanda wa Canada unaoangazia uhamiaji haramu na ulanguzi wa wahamiaji Afrika Magharibi na kusaidia kuwarejesha makwao kuungana na jamii. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM na hapa anazungumzia mantiki ya mkutano huo

(SAUTI YA JUMBE)