UM wakaribisha kuachiliwa wanasiasa Cambodia na kutaka haki ya kujieleza iruhusiwe katika uchaguzi ujao

15 Machi 2013

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na haki za binadamu kwa Cambodia, Surya P. Subedi, amekaribisha hatua ya uachiliwaji huru mwanasiasa Mam Sonando, na wakati huo huo ameonyesha matumaini yake juu ya hatua nyingine ambayo serikali inakusudia kuwachilia pia wanaharakati wengine, Kan Sovann na  Mr Touch Ream kama sehemu ya kutii uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufani Machi 14 mwaka huu.

Mtaalamu huyo amesema kuwa mahakama ya rufani iliwakuta hawana hatia watu hao ambao awali walihukumiwa kwenda jela miaka 20 kwa makosa mbalimbali ikiwemo jariobio la kufanya mapinduzi.

Amesema uamuzi wa mahakama ya rufani na hatua muhimu na ameitolea mwito serikali kuheshimu uhuru wa maoni. Taifa hilo linatazamiwa kuwa na uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu