Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasikitishwa na ripoti za ukatili dhidi ya watu wa jamii ya Rohingya kwenye boti

UNHCR yasikitishwa na ripoti za ukatili dhidi ya watu wa jamii ya Rohingya kwenye boti

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limeitaka serikali ya Thailand kutolea ufafanuzi kuhusiana na taarifa za kutoswa kwenye maji kwa boti ya Rohingya  na tukio la ufyatuaji wa risasi.

Msemaji wa UNHCR Fatoumata Lejeune-Kaba amesema kuwa maafisa wa shirika hilo wamekutana na baadhi ya manusura wa tukio hilo, lililotokea katika eneo la Phang Nga, Kusini mwa  Thailand na kubaini kuwepo kwa hali ya sintofahamu.

Imedaiwa kuwa tukio la namna hiyo limewahi kuripotiwa kutokea katika eneo la Aceh, nchini Indonesia mwezi February mwaka huu.

Maafisa wa UNHCR wamesema kuwa kuna uwezekano mkubwa tukio la ufyatuaji risasi lilifanyika wakati boti hiyo ilipozingira na kuanzisha jaribio la kuwatosa kwenye maji wasafiri wa mashua hiyo.