Hasara itokanayo na majanga ya asili yavunja rekodi 2012

14 Machi 2013

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupunguza athari za majanga (UNISDR) imesema katika historia  na kwa mara ya kwanza kabisa ulimwengu  umeshuhudia  hasara kubwa ya kiuchumi ya mwaka inayotokana na majanga kwa muda wa miaka mitatu mfululizo na kuzidi dola bilioni 100.  Ofisi hiyo imesema tathmini ya hasara ya majanga ya kiasili  tangu mwaka 1980 inaonyesha kuwa tangu miaka ya tisini kumekuwa na ongezeka la hasara ya kiuchumi na bado inazidi kuongezeka ambapo mwaka jana ilikuwa dola bilioni 138.  Mathalani asilimia 63 ya hasara hiyo ni kwa nchi za Amerika hususan kutokana na kimbunga Sandy na ukame na kwa mujibu wa ripoti hiyo bara la Ulaya lilikumbwa na misimu miwili ya baridi kali iliyosababisha vifo vya watu 1000 huku bara la Afrika likiathiriwa na ukame na mafuriko nchini Nigeria yaliyosababisha vifo vya watu 300.  Prof. Debby Guha-Sapir, ni Mkurugenzi wa kituo cha kimataifa cha taarifa za majanga na hapa anafafanua zaidi.

(SAUTI Prof. Debby)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter