Ripoti ya maendeleo ya watu yaonyesha mataifa ya Kusini mwa dunia kuinuka

14 Machi 2013

Ripoti mpya ya maendeleo ya wanadamu ya mwaka 2013 inaonyesha mabadiliko makubwa katika mienendo ya maendeleo kote duniani. Mabadiliko hayo yanatokana na kasi kubwa ya kuinuka kimaendeleo kwa nchi zinazoendelea, pamoja na umuhimu wake katika maendeleo ya wanadamu kwa ujumla.  Ripoti hiyo inasema kuwa nchi za Kusini mwa ulimwengu zinaendelea kwa kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa katika historia ya mwanadamu, huku mamilioni ya watu wakijikwamuwa kutoka katika umaskini, na mabilioni ya wengine wakitarajiwa kujiunga na tabaka la kati kiuchumi.  Kutoka barani Afrika, nchi za Ghana, Mauritius, Rwanda na Uganda zipo miongoni mwa nchi kumi na tatu zinazotajwa kuwa msitari wa mbele katika kuendelea kwa kasi zaidi. Ripoti hiyo inachanganua sababu za ukuaji wa nchi hizi na hatma ya ukuaji huo, pamoja na changamoto zinazokabiliana nazo sasa, na miongo ijayo. Khalid Malik, ni Mwandishi mkuu wa Ripoti hiyo ya maendeleo ya wanadamu:

(SAUTI YA Khalid Malik)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter