Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza laongeza muda wa UNSMIL Libya

Baraza laongeza muda wa UNSMIL Libya

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) kwa kipindi cha miezi kumi na miwili zaidi, pamoja na kulegeza vikwazo vya silaha ili kuiruhusu serikali mpya ya Libya kuweza kuagiza silaha za kutumia katika kuimarisha usalama.

Barza la Usalama limefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu hali nchini Libya. Ripoti hiyo imeaangazia hali ya kisiasa, usalama na majukumu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) inasema kwamba ingawa kuna hatua zilizopigwa katika kubadilisha mfumo wa kisiasa nchini humo, bado kuna matatizo na changamoto nyingi.

Ripoti imetaja kuenea kwa silaha haramu nchini humo kama changamoto kubwa katika kuimarisha usalama.  Ripoti hiyo imewasilishwa na Tarek Mitri, ambaye ni Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, (UNSMIL).

(SAUTI YA MITRI)