Askari wa Umoja wa Mataifa ajeruhiwa kwa risasi Sudan Kusini
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMISS umelaani shambulizi lililosababisha kujeruhiwa kwa mmoja wa askari wa kulinda amani wakati wa doria Mashariki mwa jimbo la Jonglei nchini humo.
Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduador del Buey askari huyo alijeruhiwa baada ya kundi la wanajeshi ambalo halikutambuliwa kufyatulia risasi ujumbe wa UNMISS uliokuwa unatokea Gurmuk kwenda Pibor.
Amesema hali ya majeruhi imeimarika baada ya kupelekwa Juba kwa matibabu.
Kufuatia tukio hilo msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa amezitaka kila pande kuheshimu uhuru wa watendaji wa UNIMISS wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine hususani pale wanapokuwa katika majukumu yao na kutaka wapewe ushirikiano katika kulinda raia ili kuimarisha usalama katika jimbo la Jonglei.