Rushwa ya ngono kikwazo cha maendeleo-Majaji

13 Machi 2013

Majaji wanaohudhuria mkutano kuhusu hadhi ya wanawake unaoendelea mjini New York, wamesema rushwa ya ngono ambayo ni tatizo kubwa duniani kwa sasa ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaochangia kuzorota kwa maendeleo na kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi. Mkutano huo umejadili namna ya kutatua ukiukwaji huo wa haki za binadamu unaotajwa pia kushusha viwango vya elimu. Katika mahojiano maalum na radio ya Umoja wa Mataifa Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mjaji Wanawake nchini humo, Jaji Engera Mmari-Kileo amesema wanawake ndio waathirika wakubwa na kuahidi kufikisha elimu ili kuwakwamua.

SAUTI (JAJI KILEO)

Kwa upande wake Jaji Imani Abudi amewataka wanawake kuwa wajasiri kusema wanapofanyiwa vitendo vya kuombwa rushwa ya ngono katika ngazi za kazi au shule ili kuweza kufanikisha harakati za kukomesha ukatili huo wa kijinsia.

SAUTI (JAJI IMANI)

Mkutano huo ni mfululizo wa mkutano wa kupinga ukatili dhidi ya Wanawake unaoratibiwa na Umoja wa Mataifa, na ambao unatarajiwa kukamilikia mwishoni mwa wiki hii.