Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya waliokufa vizuizini DRC 2012 yaongezeka maradufu

Idadi ya waliokufa vizuizini DRC 2012 yaongezeka maradufu

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini ongezeko kubwa la watu wanaokufa wakiwa kizuizini na magerezani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC hususan katika kipindi cha mwaka jana.  Utafiti huo uliofanywa na ofisi yaTume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini DRC katika vituo kadhaa, umebainisha hali mbaya iliyopo kwenye vituo hivyo hali ambayo inazidisha wasiwasi kwa wanaoshikiliwa.Kulingana na utafiti huo, katika kipindi cha Januari 2010 hadi Disemba mwaka 2012, jumla ya raia 211 walipoteza maisha wakiwa mikononi mwa dola. Na mwaka jana  pekee, kiasi cha watu waliopoteza maisha kinaarifiwa kufikia 101, ikiwa na ongezeko la mara mbili ikilinganishwa na vifo vilivyoripotiwa katika kipindi cha mwaka 2010 na 2011. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE)