Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu mwenendo wa idadi ya watu duniani wamalizika

Mkutano kuhusu mwenendo wa idadi ya watu duniani wamalizika

Mkutano wa viongozi wa serikali  kutoka nchi 51 umekamilika leo nchini Bangladesh. Majadiliano ya mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa kwa ushirikiano wa nchi hiyo na Uswisi, yalihusu  mienendo ya  idadi ya watu duniani, likiwemo suala la uhamiaji. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM William Swing aliyeko Bangladesha kwa ziara ya siku tatu alihudhuria mkutano huo ambao  ni sehemu ya mfululizo wa mijadala Kumi na Moja ya Umoja ya Mataifa iliyoandaliwa kote duniani kuhusu mada hiyo.

Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM na anaelezea jinsi uhamiaji unavyochangia katika mienendo ya idadi ya watu na maendeleo.

(SAUTI YA JUMBE)