Ban aomboleza vifo vya marubani nchini Kongo DRC.

12 Machi 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amepokea kwa masikitiko habari za vifo vya marubani wanne wa Urusi kufuatia ajali ya ndege ya kukodi ya mizigo ya Umoja wa Mataifa iliyoanguka kilometa 20 Mashariki mwa DRC Kongo katika mji wa Kivu Machi 9 mwaka huu.

Kufuatia vifo hivyo, Bwana Ban ametuma salamu za rambirambi na pole kwa familia, marafiki na serikali ya Shirikisho la Urusi walikotoka  marubani hao walioptoeza maisha.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kongo DRC MONUSCO ulianzisha uchunguzi na uokozi wa haraka ambapo hata hivyo kutokana na hali mbaya ya hewa ujumbe huo haukuweza kufika katika eneo la tukio hadi March 12. Uchunguzi wa sababau za ajali hiyo unaendelea.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud