Mamilioni wakabiliwa na njaa Malawi-FAO

11 Machi 2013

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva amesema licha ya kwamba Malawi imepiga hatua katika uzalishaji wa mahindi, uhakika wa chakula na hata kusafirisha nje nafaka hiyo bado watu milioni mbili nchini humo hawana uhakika wa chakula.

Mkurugenzi huyo mkuu wa FAO na Kamishna wa Maendeleo ya Umoja wa Ulaya Andris Piebalgs waliongoza ujumbe wa pamoja wa EU na FAO nchini humo na kujadiliana na serikali jinsi ya kusaidia serikali kuongeza usalama wa chakula kilimo endelevu.

Graziano da Silva amesema FAO inaamini kuwa wakulima wadogo wadogo wakijiunga katika vikundi vya ushirika  wanaweza kujikomboa katika umaskini na utapiamlo kwa kuboresha uwezo wao wa ufikiaji masoko, ununuzi wa pembejeo kw abei nafuu na kupata huduma za mikopo na hifadhi ya kijamii.

(SAUTI YA GRAZIANO)

 “ Hoja ya pili ni kwamba kwa bahati mbaya Malawi bado ina idadi kubwa ya watu wenye utapiamlo licha ya kuongeza kiwango cha kuzalisha mahindi .Tunasadia nchi hii na tunatafuta njia ya kuendeleza mipango ya chakula kuwaondoa watu na umaskini na tunaamini hi ndio njia muafaka.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter