Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka miwili baada ya ajali ya Fukushima, IAEA yahakikisha usalama wa nyuklia

Miaka miwili baada ya ajali ya Fukushima, IAEA yahakikisha usalama wa nyuklia

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki  IAEA Yukiya Amano amesema miaka miwili baada ya tsunami nchini Japani lililosababisha ajali katika mtambo wa nyuklia wa Fukushima Daiichi nchini humo, shirika lake linaendelea kushirikiana na nchi hiyo kuimarisha usalama kwenye mitambo.  Ametoa tamko hilo leo ikiwa ni kumbukumbu ya miaka miwili tangu tetemeko hilo la chini ya ardhi mwaka 2011lililosababisha kuvuja kw nyuklia kwenye mtambo wa Fukushima na uharibifu wa mali na vifo vya watu.

Halikadhalika amesema nchi zinaendelea kuzingatia viwango vya usalama vya nyulia na kwamba shirika hilo limesambaza wataalamu kwa nchi wanachama wa shirika hilo kuangalia usalama wakati wa uendeshaji, mifumo ya udhibiti na uchukuaji  hatua pindi kunapoibuka tatizo.  Bwana Amano amesema nchi wanachama 159 wa IAEA zimepiga hatua kuhakikisha usalama wa Nyukilia kwa kuzingatia makubaliano yaliyotiwa saini mwezi Septemba mwaka 2011 na ameeleza kuwa IAEA itaendelea kupitia na kuimarisha viwango vya usalama vya nyuklia.