Ban apongeza wakenya, azungumza na Uhuru na Raila

10 Machi 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameona matokeo ya uchaguzi mkuu wa Kenya yaliyotangazwa na Tume ya Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo IEBC na kuwapongeza wakenya kwa azma yao waliyoonyesha ya kushiriki uchaguzi ho kwa amani na uvumilivu wao wakati wakisubiri matokeo.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa tayari Bwana Ban amezungumza kwa njia ya simu na Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Katika mazungumzo yake na Kenyatta na Uhuru, Bwana Ban amesisitiza wito wake kwao wa kuwataka kupeleka ujumbe dhahiri wa utulivu kwa wafuasi wao. Halikadhalika amewakumbusha ahadi zao walizotoa wakati wa mchakato mzima wa kuwasilisha pingamizi zozote za uchaguzi kwa njia za kisheria.

Kwa mantiki hiyo, Katibu Mkuu amesifu matamko yao waliyotoa mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa na kueleza kuwa wakati huu wananchi wa Kenya wanahitaji uongozi wenye busara na unaowajibika.

Kwa mujibu wa IEBC, Uhuru amepata asilimia 50.07 ya kura zote halali zilizopigwa huku Odinga akipata asilimia 43.3.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter