Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Askari 21 wa UNDOF wako salama: Ladsous

Askari 21 wa UNDOF wako salama: Ladsous

Msimamizi mkuu wa shughuli za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous amelieleza baraza la Usalama kuhusu hali ya walinzi wa amani 21 wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo kwenye maeneo huru ya uangalizi, UNDOF huko Golan, ni salama na kwamba jitihada zinaendelea ili waweze kuachiwa huru.  Akitoa muhtasari kwa waandishi wa habari, Ladsous amesema walinzi hao wa amani 21 wamegawanywa katika makundi matano kwenye kijiji kimoja  na kuna matarajio ya kuwepo kwa kusitishwa mapigano kwa saa chache ili waweze kuachiwa huru.