Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi wahama makwao nchini Syria: WFP

Watu zaidi wahama makwao nchini Syria: WFP

Mapigano yanayoendelea kushuhudiwa kwenye jimbo la Raqqah kaskazini mashariki mwa Syria yamechangia kuhama kwa watu upya wakati zaidi ya familia 20,000 zinapohama makwao na kukimbila jimbo la Deir Ezzor. Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limetuma malori matatu yaliyosheheni chakula kwa watu 20,000 kwa muda wa siku tatu zilizopita kitakachosambazwa kwa familia zilizohama makwao zilizo piga kambi kwenye jimbo la Deir Ezzor. Malori mengine matano kwa yanajazwa chakula ambacho kitapelekewa wale waliohama makwao. Huku idadi ya wakimbizi wa Syria ikipita watu milioni moja WFP inaongeza mikakati yake ya dharura mwezi huu kuwalisha watu 800,000 kwenye nchi majirani mwezi huu wa Machi ingawa msemaji wa WFP, Elizabeth Byrs anasema wanakumbana na changamoto ya jinsi ya kuwafikia wengi wa wakimbizi