Uchunguzi wa angani wabaini kuzorota kwa usalama huko Kivu Kaskazini: IOM

8 Machi 2013

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, limesema watu 75,000 wamekimbia makazi yao kwenye jimbo la Kivu Kaskazini huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC kufuatia mapigano yaliyoubuka hivi karibuni katika eneo la Kitchanga, lililopo karibu na mji wa Masisi, takribani kilomita 80 magharibi mwa mji wa Goma.  Taarifa hizo ni kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na vyombo maalum angani ambapo imeelezwa kuwa mapigano makali  baina ya vikosi vya serikali  na muungano wa kundi la waasi wa linalopigania uhuru wa Congo APCLS, yalizuka tena hivi karibuni na kusababisha mamia ya watu kukosa makazi.  Inakadiriwa kwamba kiasi cha watu 80 wamepoteza maisha na zaidi ya nyumba 300 zimeharibiwa kufuatia mapigano hayo ambayo yamekuja licha ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwezi uliopita huko Addis Ababa, Ethiopia.  Jumbe Omar Jumbe ni msemaji wa  IOM

(SAUTI YA JUMBE)