Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aunga mkono vikwazo dhidi ya DPRK

Ban aunga mkono vikwazo dhidi ya DPRK

Katika taarifa ambayo ameitoa mara tu baada ya kura ya Baraza la Usalama, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha azimio hilo na kusema ya kwamba, kwa kulipitisha kwa kauli moja, Baraza la Usalama linatuma ujumbe kinaga ubaga kwa DPRK ya kwamba, jamii ya kimataifa haitokubali juhudi zake za kuendeleza silaha za kinyuklia na vitendo vinavyohusika navyo.

Azimio hilo la Baraza la Usalama linaiwekea DPRK vikwazo vya kifedha, na litahitaji nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha taifa hilo haliwezi kutuma au kupeleka fedha kulipia vifaa vya kutengeneza zana zake za nyuklia.

Azimio hilo pia limewawekea vikwazo vya kusafiri maafisa wa Korea Kaskazini ambao wanahusika na biashara ya vifaa vya kinyuklia au kueneza teknolojia ya zana za kinyuklia pamoja na vikwazo vya kuzuia bidhaa za anasa kwa DPRK

Bwana Ban amesema kwa azimio hilo, Baraza la Usalama limeendeleza mwenendo wa kimataifa unaopinga majaribio yoyote ya kinyuklia na kuimarisha makubaliano ya kutoeneza silaha hizo.

Ametoa mwito kwa DPRK na mataifa wanachama wa Umoja wa Mataifa kutekeleza matakwa ya azimio hilo.