Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yatoa ulinzi kwa raia waliokimbilia ofisi yake Sudan Kusini

UNMISS yatoa ulinzi kwa raia waliokimbilia ofisi yake Sudan Kusini

Zaidi ya watu 2,500 wamekimbilia makao ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini (UNMISS) Jumatano asubuhi kufuatia mapigano yalozuka kati ya kundi moja lenye silaha na wanajeshi wa serikali, SPLA, karibu na soko la Pibor, kwenye jimbo la Jonglei.  Kwa kuitikia matukio hayo, UNMISS imewatuma wanajeshi wake wa kulinda amani kusaidia kuwalinda raia katika eneo hilo. Hivi sasa hali imetulia tena, na raia wamerudi makwao. Hata hivyo, UNMISS imesema itaendelea kufanya kila iwezalo ili kuwalinda raia katika eneo hilo