Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakenya hitimisheni uchaguzi kwa amani: Ban

Wakenya hitimisheni uchaguzi kwa amani: Ban

Wakati raia wa Kenya wakisubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi wa mapema wiki hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kukamilisha shughuli za uchaguzi kwa amani na njia inayoaminika itakuwa hatua muhimu katika demokrasia ya Kenya.

Bwana Ban amesema kwamba ametiwa moyo kuona shughuli ya uchaguzi ikiendeshwa kwa njia ya amani na taratibu, licha ya matukio machache ya ghasia na matatizo ya kiteknolojia.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa wale walopiga kura, pamoja na wanasiasa walochuana kwenye kura hiyo na wafuasi wao kuwa watulivu na wenye subira, ili wairuhusu tume ya uchaguzi kukamilisha kazi yake ya kuhesabu kura.