Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuendeleza ushirikiano na Venezuela

UM kuendeleza ushirikiano na Venezuela

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesisitiza tena kuwa Umoja huo utaendelea kuunga mkono jitihada za Venezuela za maendeleo na ustawi. Bwana Ban amesema hayo katika salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa nchi hiyo Hugo Chavez.  Katika salamu hizo pamoja na kuelezea kushtushwa na kifo cha Rais Chavez, Bwana Ban amemzungumzia kiongozi huyo na kusema alikuwa mwenye dira na mstari wa mbele kuzungumzia changamoto na matarajio ya watu walio maskini nchini mwake.  Halikadhalika Bwana Ban amesema mchango wa marehemu Chavez pia katika amani kwenye nchi za Amerika Kusini hautasahaulika akigusia jinsi alivyochochea harakati za ushirikiano wa kikanda kwenye eneo lao na mazungumzo ya sasa ya amani kati ya serikali ya Rais Juan Manuel Santos wa Colombia na waasi wa kikundi cha FARC. Wakati huo huo wajumbe wa Baraza la Usalama hii leo asubuhi kabla ya kuanza kwa kikao walisimama na kuwa kimya kwa dakika moja kumkumbuka marehemu Chavez