Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atuma rambi rambi zake kufuatia kifo cha Chavez

Ban atuma rambi rambi zake kufuatia kifo cha Chavez

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametuma ujumbe wa rambi rambi kwa familia na watu wa Venezuela kufuatia kifo cha rais wao, Hugo Chavez.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, Bwana Ban ambaye amekiri ya kwamba ndio kwanza alikuwa anasikia habari za kifo cha Chavez katika mkutano huo nao, amemsifu Marehemu Chavez kama mtu aliye changia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi yake.

Bwana Ban amesema atatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hilo la huzuni.