Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay ashutumu mauwaji wa walemavu wa ngozi Tanzania, ataka wahusika wachukuliwe hatua.

Pillay ashutumu mauwaji wa walemavu wa ngozi Tanzania, ataka wahusika wachukuliwe hatua.

Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya Haki za binadamu Navy Pillay ameitaka serikali ya Tanzania kuchukua hatua za hataka kukomesha vitendo vya mauwaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Amesema kuwa amevunjwa moyo na kusikitishwa juu ya taarifa za kukithiri kwa mauwaji kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, na hivyo kutoa mwito kwa serikali kuhakikisha wahusika wa matukio hayo wanasakwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Kumekuwa na taarifa ya kujiri mara kwa mara kwa watu wanaodaiwa kuwa na imani za kishirikiana wanaoendesha kampeni za kuwavamia watu wenye ulemavu huo wa ngozi

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTI YA RUPERT C)