Sheria kikwazo katika kutokomeza ukatili kwa wanawake

5 Machi 2013

Kutokuwepo kwa  sheria zinazoainisha ukatili kwa wanawake majumbani ni kikwazo katika kupambana na ukatili kwa wanawake.

Mkuu wa Kitengo cha maswala ya Jinsia na kuwawezesha wanawake katika Umoja wa Mataifa   MICHELLE BACHELET amesema hadi sasa ni nchi 125 pekee ulimwenguni ambazo sheria zake zinaweka bayana kwamba ukatili wa majumbani ni kosa la jinai huku nchi nyingine 600 sheria zake haziainishi ukatili wa majumbani kama kosa la jinai jambo linalochangia ukatili huo kwa wanawake kuendelea.

Bibi Michelle amesema serikali ni chombo muhimu katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia ambao unaathiri zaidi wanawake na wasichana kote ulimwenguni.

Kadhalika amesema ukatili sio tu kwamba unadumaza familia lakini pia ni kikwazo kwa maendeleo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter