Matatizo ya mifumo ya afya yawatia akina mama waja wazito nchini Mali hatarini kifedha

4 Machi 2013

Mamia ya familia nchini Mali wanakabiliwa na jinamizi la kupoteza fedha nyingi wakati wa zoezi la kujifungua kwa kina mama kutokana na kukosekana kwa vifaa maalumu ambavyo vinaweza kuokoa maisha ya mama.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa katika jarida la shirika la afya ulimwenguni WHO, pamoja na kuwepo kwa juhudi za kuwepo kwa huduma za kuhakikisha uhai wa mama, lakini kumejitokeza tatizo kubwa ambalo linakwaza ustawi wa afya nchini humo.

Hali hiyo inayojitokeza Mali ni mfano wa matatizo kama hayo yanayoziandaama nchi nyingi ambazo zinakabiliwa na vifaa maalumu kwa ajili ya kugharimia usalama wa mama wakati wa kufifungua. George Njogopa na taarifa kamili:

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)