Biashara haramu yaipora Afrika nyani 3000 kila mwaka: UNEP

4 Machi 2013

Biashara haramu ya nyani inaipokonya misitu ya bara la Afrika na Asia Kusini takriban nyani 3000 kila mwaka na inatajwa kuongezeka na kuwa kitisho kwa idadi ya nyani maeneo hayo, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP.

Ripoti hiyo yenye kichwa “Nyani Walioibwa” ndiyo ya kwanza kuangazia bishara hiyo haramu na mitandao inayohusika ambayo idara zinazohusika na sheria zinajaribu kukabiliana nayo. Jason Nyakundi na taarifa kamili

(Ripoti ya Jason Nyakundi)