Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran, Korea Kaskazini na Japan zamulikwa kwenye mkutano wa halmashauri ya IAEA

Iran, Korea Kaskazini na Japan zamulikwa kwenye mkutano wa halmashauri ya IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, (IAEA) Yukiya Amano, amesema shirika hilo linaendelea kujitahidi kuisaidia Japan kukabiliana na athari za ajali ya nyuklia ilotokea nchini humo yapata miaka miwili ilopita.

Akiuhutubia mkutano wa halmashauri ya magavana wa shirika la IAEA, Bwana Amano ametoa ripoti kuhusu suala la kuhakiki usalama wa mpango wa nyuklia nchini Iran, akisema kwamba hadi sasa, shirika hilo haliwezi kuhakiki ikiwa mpango wa nyuklia wa Iran ni kwa ajili ya matumizi ya amani.

Halmashauri hiyo yenye uanachama wa nchi 35 inakutana kujadili kazi ya IAEA ya kuhakiki mipango ya nyuklia, usalama, na matumizi ya amani ya teknolojia ya nyuklia. Bwana Amano ameelezea kusikitishwa kwake na jaribio la silaha za nyuklia lilofanywa na Jamhuri ya Korea Kaskazini, DPRK.

(SAUTI YA AMANO)