Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAIDS yakaribisha habari za mtoto “kupona” baada ya matibabu dhidi ya HIV

UNAIDS yakaribisha habari za mtoto “kupona” baada ya matibabu dhidi ya HIV

Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa juu ya ugonjwa wa Ukimwi (UNAIDS) leo umekaribisha ripoti ya utafiti kuhusu mtoto aliyetibiwa kwa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi saa thelathini baada ya kuzaliwa na kisha kuacha matibabu hayo lakini akapatikana hana tena maambukizi.

Kwa mujibu wa utafiti huo mama mzazi wa mtoto huyo hajawahi kupata tiba ya kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi. Ripoti ya utafiti huo itawasilishwa leo katika kongamano juu ya Maambukizi na Kinga mjini Atlanta, Georgia nchini Marekani. Taarifa zaidi na Joseph Msami