Uchaguzi wa Kenya mwaka 2013

1 Machi 2013

Mnamo Siku ya Jumatatu tarehe nne mwezi Machi mwaka huu wa 2013, wananchi wa Kenya watajitokeza kutimiza wajibu wa kimsingi kisiasa. Siku hiyo, Wakenya watapiga kura kumchagua rais mpya, na viongozi wengine, ambao wataendesha gurudumu la kisiasa nchini humo kwa kipindi kingine cha miaka mitano.

Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu sana uchaguzi huo, kwani Uchaguzi uliopita wa mwaka 2017, uliibua machafuko, ambayo yaliyakatili maisha ya zaidi ya watu elfu moja, na kuwaacha wengine zaidi ya 3,000 bila makazi. Je, hali imebadilika? Ili kutathmini hilo, na nafasi ya vijana katika kuendeleza demokrasia na maendeleo, ungana naye Joshua Mmali akizungumza na vijana wa chuo kikuu cha United States International University (USIU) kilichoko huko Nairobi, Kenya, ambao wametembelea studio zetu baada ya kushiriki kwenye kongamano la vijana linaloiga muundo wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.