Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kufungwa mpaka wa Iraq kwayatia mashirika ya misaada wasiwasi

Kufungwa mpaka wa Iraq kwayatia mashirika ya misaada wasiwasi

Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yameelezea kusikitishwa na hatua ya Iraq kuufunga mpaka wa Al-Qa’im kati yake na Syria, ingawa unafunguliwa kwa ajili ya huduma za matibabu ya dharura.

Raia wa Syria zaidi ya milioni moja  ambao wameshavuka mpaka na kukimbilia nchi jirani wanahitaji msaada wa kibinadamu kama huduma za afya na malazi huku pia swala la kufungwa kwa mpaka wa Iraq likiendelea kuzua mjadala.

Misaada zaidi ya kidharua inahitajika ili kusaidia wanawake na watoto ambao ni asilimia 66 ya wakimbizi wa Syria, ambayo imekumbwa na machafuko kufuatia mapigano kati ya seriakali na waasi. Hata hivyo, mashirika ya misaada yamepokea tu asilimia 19 tu ya ombi la ufadhili kwa ajili ya Syria.