Sheria na haki vyaangaziwa na Kamati ya kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake

1 Machi 2013

Kamati ya kutokomeza unyanyasaji wa Wanawake imekamilisha kikao chake cha 54 kwa kurithia ripoti saba za mapendekezo yake kuhusu haki za wanawake na sheria za kulinda haki hizo, kwa lengo la kutoa mwongozo wa kuendeleza haki za wanawake na uwezo wao kupata haki. Mapendekezo hayo yanahusu hatua stahiki za kuchukua kuhakikisha kwamba haki za wanawake zinalindwa katika nchi nane, zikiwemoAngola,AustrianaPakistan.

Wanenaji mwishoni mwa kikao hicho cha wiki tatu wamesema mapendekezo hayo yatakuwa kielelezo katika kusaidia mataifa hayo kuondoa vikwazo ambavyo wanawake hukumbana navyo wakati wakijaribu kutafuta haki ambazo zimewekwa kwa mujibu wa sheria.

Mbali na kujadili harakati za kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake, pia kamati hiyo ilifanya mikutano na mshirika yasiyo ya kiserikali, taasisi za kitaifa za haki za binadamu na wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter