UNESCAP waibua matumaini mapya Asia na Pasific

UNESCAP waibua matumaini mapya Asia na Pasific

Mkutano wa  hivi punde uliojikita katika  kukuza maendeleo katika ukanda wa Asia na Pasific umeibua matumaini mapya kwa nchi mweneyeji wa mkutano huo Timor- Leste .

Akiongea baada ya mkutano huo Waziri Mkuu wa nchi hiyo JOSE GUSMAO amesema kasi ya maendeleo katika bara la Asia yamethibitisha kwamba bara hilo linaweza kuandikia historia mpya kwa kuzingatia kutimiza kwa upya malengo ya Milenia yanayofikia kikomo mwaka 2015.

Kongamano hilo lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa kuhusu mswala ya kiuchumi nakijamii kwa maeneo ya Ashia na Pasific UNESCAP umefanikisha kusikia saiti za ukanda wa Asia na Pasifiki kuhusu namna bora ya kutimiza Malengo ya Milenia na mipango ya baada ya malengo hayo.