Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya Haki za Binadamu ya UM kupeleka waangalizi kwa uchaguzi wa Kenya

Ofisi ya Haki za Binadamu ya UM kupeleka waangalizi kwa uchaguzi wa Kenya

Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, imesema itapeleka timu ya waangalizi wa haki za binadamu nchini Kenya katika siku chache, ambao watakuwemo nchini humo wakati wa shughuli nzima ya uchaguzi.

Akitangaza hilo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva, msemaji wa afisi hiyo ya haki za binadamu, Rupert Colville, amesema waangalizi hao wanne watafuatilia hali ya haki za binadamu wakati wa uchaguzi, pamoja na kuisaidia tume ya kitaifa ya haki za binadamu nchini humo na mashirika ya umma.

Uchaguzi uliopita mwaka wa 2007 ulifuatiwa na machafuko yalosababisha vifo vya zaidi ya watu elfu moja, na kuwaacha wengine zaidi ya elfu tatu bila makazi. Ili kujua ikiwa Wakenya wa tayari kudumisha amani wakati wa uchaguzi, tulipata maoni ya baadhi yao mitaani Nairobi

(MAONI Kenya)