Skip to main content

Juhudi zaidi zahitajika kutimiza malengo ya Milenia

Juhudi zaidi zahitajika kutimiza malengo ya Milenia

Imeelezwa kwamba mipango ya maendeleo ya sasa duniani lazima ijikite katika njia bora zenye uwiano wa kutimiza malengo ya Millenia yanayofikia kikomo mwaka 2015.

Akitoa hutuba ya ufunguzi wakati wa kongamano lililopewa jina Tendea kazi malengo ya Milenia,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo UNDP amesema changamoto za uchumi kama vila upatikanaji wa chakula,mafuta, pamoja na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi na siasa zimetoa mtizamo mpya wa namna uchumi unavyoweza kuwa mgumu na kuwa kikwazo cha kutimiza malengo.

Bi Clerk amesema hata hivyo malengo ya Milenia yametoa somo juu ya namna ya kuwa na malendo ya juu kufikiri maradufu kwa kiwango cha juu cha mipango ili kutimiza lengo.

Mkurugenzi huyo wa UNDP amesema makakati wa baada ya kufikia malengo ya milenia mwaka 2015 unahitaji kuwa kivuli cha malengo mapya na utekelezajai huku pia akiweka wazi kwamba mengi yamefanyika tangu kutiwa saini kwa Malengo ya Milenia yanayofikia kikomo.

Mkutano huu unafanyika zikiwa zimebaki siku elfu moja kabla ya dec 31 2015 ambao ndio mwisho wa utekelezaji wa Malengo ya milenia.Nhi 189 zilikubali kutia saini makubaliano hayo yenye malengo mengi ikiwemo Upatikanaji wa uhakika wa majina k upambana na njaa.