Hatari ya saratani ipo juu tu kwenye maeneo yaloathiriwa na ajali ya nyuklia Fukushima: WHO

28 Februari 2013

Uchunguzi wa kina uliofanywa na wataalam wa kimataifa kuhusu hatari za kiafya kutokana na ajali ya kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Fukushima Daiichi nchini Janapan, umebaini kuwa hatari zilizotarajiwa kwa ujumla ndani na nje ya Japan zipo chini, na kwamba hakuna dalili zozote za kuongezeka viwango vya hatari hizo kuzidi viwango vya kawaida.

Hata hivyo, ripoti hiyo ya Shirika la Afya Duniani, WHO inayohusiana na uchunguzi huo wa ajali ilotokana na tetemeko la ardhi na tsunami mwaka 2011, imesema kuwa makadirio ya hatari ya aina fulani za saratani miongoni mwa watu wanaoishi katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Fukushima imeongezeka, na hivyo kutoa wito wa uchunguzi wa muda mrefu na upimaji wa watu hao.

Uchunguzi huo wa wataalam ulinuia kufanya makadirio ya hatari kwa watu wa Fukushima, kote nchini Japan na kwingineko duniani, pamoja na kwa wafanyakazi na wale walokuwa kwenye kiwanda hicho kutoa huduma za dharura.

Dr Maria Neira, Director, ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Umma na Mazingira katika WHO

(SAUTI YA DR. NEIRA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter