Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumaliza ugonjwa wa ukimwi ni suala la haki za binadamu:UNAIDS

Kumaliza ugonjwa wa ukimwi ni suala la haki za binadamu:UNAIDS

Mkurugernzi mkuu wa programu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na virusi vya HIV na ugonjwa wa ukimwi UNAIDS, Michel Sidibe, amesema kuwa kumaliza tatizo la ugonjwa wa ukimwi ni haki ya binadamu kwa wote.

Akihutubia baraza la haki za binadamu la  Umoja wa Mataifa juu ya suala la kutokuwepo usawa katika jitihada za kupamaba na ugonjwa wa ukimwi Sidibe amesema kuwa wanadamu wote wana haki sawa ya kuishi , afya na usalama.

Amesema kuwa ni aibu kwamba mwaka kama huu wa 2013 ambapo kuna njia zote za kumaliza ugonjwa huu, bado watu miliono 1.7 wanaendelea kuaga dunia kila mwaka kwa kukosa kupata matibabu.

Ameongeza kuwa ni asilimia 28 ya watoto tu ndio hupokea matibabu kati ya wanaoihitaji akiongeza kuwa mikakati ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi  ni chombo ya kumaliza kutokuwepo usawa kati ya maskini na matajiri.

(SAUTI YA SIDIBE)