Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mataifa yaanza kupiga hatua kukabiliana na uvuvi haramu

Mataifa yaanza kupiga hatua kukabiliana na uvuvi haramu

Hatimaye mataifa mbalimbali duniani yameanza kupiga kahatua kuridhia mpango wenye shabaha ya kukabiliana na wimbi la uvuvi haramu ambao unafanywa bila kuzingatia vigezo vya kimataifa na hatua hiyo inafuatia majadiliano yaliyofanywa kwa miaka kadhaa.

Vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vimekithiri katika maeneo mbalimbali vinatajwa kusababisha uharibifu wa viumbe hai pamoja na uoto wake wa asili.

Lakini sasa kumefaulu kupitishwa mpango mkakati ambao unatoa mwongozo kwa mataifa duniani kudhibiti na kusimamia mienendo ya uvuvi harama kw a lengo la kuvinusuru viumbe hai. Mwongozo huu huo unahimiza kuwepo kwa dhana ya uwajibikaji na kwa nchi ambazo husajili meli za uvuvi. George Njogopa na maelezo zaidi:

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)