Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni ya watu kwa sasa wanakabiliwa na matizo ya kusikia duniani :WHO

Mamilioni ya watu kwa sasa wanakabiliwa na matizo ya kusikia duniani :WHO

Zaidi ya watu milioni 360 duniani wanakabiliwa na tatizo la kupoteza uwezo wa kusikia kwa mujibu wa makadirio yaliyotolewa na Shirika la afya duniani WHO kabla ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kulea sikio ambayo itadhimishwa tarehe tatu mwezi ujao wa Machi. Huku watu wakiendelea kupatwa na uzee duniani visa vya wao kukabiliwa na tatizo la kusikia vinazidi kuongezeka.

Mtu mmoja kati ya watu watatu walio na zaidi ya miaka 65 ikiwa ni jumla ya watu milioni 165 duniani kwa sasa hawana uwezo wa kusikia. Hata kama tatizo la kusikia linaweza kutatuliwa na vifaa vinavyosaidia kusikia bado vifaa ni adimu ikilinganishwa na watu wanaovihitaji. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA JASON)