Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na washirika wakomboa watoto kutoka ajira migodini huko DRC

UNICEF na washirika wakomboa watoto kutoka ajira migodini huko DRC

Ajira kwa watoto watoto ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazokabili nchi zinazoendelea. Katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC hali ni mbaya zaidi. Nchini humo sio ajabu kuwaona  watoto wenye umri wa kwenda shule wakifanya kazi za kujipatia kipato ambazo hata hivyo huwaingizia kipato kidogo  ikilinganishwa na kazi wanazofanya. Mwenzangu JOSEPH MSAMI anamulika adha wanazokutana nazo watoto wanapokuwa katika migodi ya uchimbaji almasi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC, ambayo ndiyo nchi yenye almasi  nyingi zaidi duniani.