Dola Milioni 45 zahitajika haraka kuokoa wanawake na watoto Mali: UNICEF

26 Februari 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa ombi la dharura la dola Milioni 45 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na watoto waliojikuta katikati ya mzozo nchini Mali kupata mahitaji ya kimsingi kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.  UNICEF inasema kuwa athari za mzozo unaoendelea kwa watoto ni kubwa mno ikitaja suala la uhaba wa lishe bora na ya kutosha, na kwamba mwaka huu yakadiriwa watoto Laki Nne Nusu wenye umri wa chini ya miaka mitano watakumbwa na utapiamlo huku Laki Mbili wakikumbwa na unyafuzi.  Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA MARIXIE)

 

“Fedha tunazoomba zitasaidia mpango jumuishi wa kukabiliana na tatizo la lishe, hii ina maana pamoja na hatua madhubuti za kuboresha lishe, mpango utajumuisha kuwaptia maji safi na salama watu wakimbizi, pamoja na kinga dhidi ya magonjwa kama vile Malaria, kipindupindu na mengineyo yasababishwayo na maji machafu. Kuboresha huduma za elimu na ulinzi pia ni sehemu ya mpango huo.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter