Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atoa wito kwa vijana kuongoza katika kuendeleza amani na maendeleo

Ban atoa wito kwa vijana kuongoza katika kuendeleza amani na maendeleo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo ya kwamba ulimwengu utategemea ujasiri na hatua mathubuti za vijana katika kutafuta amani na maendeleo endelevu.

Bwana Ban amesema hayo mjini Vienna, Austria, akikutana na vijana wakati wa mkutano wa tano wa kimataifa wa nchi zinazotetea ustaarabu, yaani Alliance of Civilizations.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa vijana waongee lugha ya kustahimiliana na heshima, na kupaaza sauti zao ili zizamishe sauti za wale wanaohubiri migawanyiko na chuki.

Ameongeza kuwa mizozo inabaki kuwa pingamizi kubwa kwa maendeleo, wakati ulimwengu ukikaribia kuanza kuhesabu siku elfu moja hadi kufikia tarehe ya malengo ya maendeleo ya milenia, na kutoa wito kwa vijana wasaidie kuongoza njia kuepuka mizozo na kufikia malengo hayo.